|
AFRIKA!
Afrika watu
Wanapenda zaidi ya kuchuki,
Wanaimba zaidi ya kulia,
Wanacheza ngoma zaidi ya mapigano,
Wanafurahi zaidi ya kukasirika,
Huchangamka zaidi ya kuhuzunika,
Bara la Afrika ni,
Tajiri kuliko masikini
Watu wake hucheka
Na hufurahia maisha,
Ndio,katika Afrika,
Pia jua huangaza.
|